Friday, February 6, 2009

Last day in the Internet Workshop.


Hawa ni washiriki wa mafunzo ya Internet wakiwa makini Darasani wakipekuwa vitu kwenye tovuti. kwa picha ya juu na ya chini yake.


Internet Workshop.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa waandaaji wa kozi hii,MISA-tanzania na VIKES foundation (Finnish Foundation for Media, Communication and Development) inayohusu mtandao, pia shukrani nyingi na za pekee zimwendee mwendeshaji wa mafunzo haya Bw. Peik Johansson, bila kumsahau Maggid Mjengwa kwa ujuzu aliotuongezea katika suala zima la matumizi ya tovuti(mtandao, Internet)

Katika kozi hii nimejifunza mengi kutoka kwa wataalamu wetu na kwa wanasemina wenzangu, ninahakika hiki nilichopata nitaweza kuwafundisha wengine ofisini kwangu ikiwa ni pamoja na kukifanyia kazi ili nisiwe nyuma ya wakati, kwa kuwa nimebaini zaidi sasa, Dunia imekuwa na mabadiliko kila siku hasa kutokana na teknolojia hii mpya.

Workshop ni fupi lakini ili kuwa na mambo mengi ya kujifunza hasa kwangu mimi ambaye sikuwahi kushiriki katika workshop kama hii ambayo kwangu ilikuwa ni mara ya kwanza ila nimeweza kujifunza, mengi ikiwa ni pamoja na kufungua tovuti yangu, kutafuta habari kupitia media zingine, nimejifunza pia kutafuta habari za michezo, na kujua website zingine, kuedit picha na kuzipeleka kwenye website.

Kutokana na haya yote ninahakika sitaweza kuyasahau ila kujituma niweze kufahamu mengi zaidi.

Mapendekezo nitafurahi iwepo mafunzo kama haya watayapata wengine pia hasa wanahabari, ili itusaide kuwa na upana wa mawazo hasa katika kutafuta habari kwa njia ya Internet.


Thanks.

No comments:

Post a Comment